JangaUlaya
Uhispania: Zaidi ya dola bil 10 kusaidia waathiriwa mafuriko
5 Novemba 2024Matangazo
Sanchez amesema kwamba serikali yake inatarajia kutumia hadi yuro milioni 838 kuwapa fedha mkononi walioathirika na mafuriko hayo yaliyosababisha vifo vya watu 217 wiki iliyopita, katika janga baya zaidi kuwahi kuikumba Uhispania.
Soma pia:Uhispania yaongeza idadi ya wanajeshi kusaidia uokoaji janga la mafuriko
Waziri Mkuu huyo amesema kuwa shirika la mikopo la serikali ya Uhispania, ICO, litatoa dola bilioni 5 kama mikopo kwa kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kadri, watu waliojiajiri na familia kwa ajili ya kufadhili ujenzi wa nyumba zao zilizoharibiwa.
Sanchez amesema Uhispania imewatuma karibu maafisa 15,000 na majeshi katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko hayo.