1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania yatinga fainali ya Kombe la Dunia, yaibwaga Sweden

15 Agosti 2023

Uhispania itacheza fainali yake ya kwanza ya Kombe la Dunia la Wanawake baada ya bao la Olga Carmona katika dakika ya 89 kuwanyanyua kina dada hao wa La Roja kwa ushindi wa 2 -1 dhidi ya Sweden katika nusu fainali

Fußball-WM Frauen - Spanien - Schweden
Picha: Brett Phibbs/AAP/IMAGO

Uhispania itacheza fainali yake ya kwanza ya Kombe la Dunia la Wanawake baada ya bao la Olga Carmona katika dakika ya 89 kuwanyanyua kina dada hao wa La Roja kwa ushindi wa 2 -1 dhidi ya Sweden katika nusu fainali.

Uhispania, ambayo mwaka jana ilikuwa na uasi kikosini kutoka kwa wachezaji dhidi ya kocha Jorge Vilda, itacheza na mshindi wa mechi kati ya mwenyeji mwenza wa mashindano hayo Australia na England katika fainali ya Jumapili mjini Sydney.

Soma pia: Sweden kulimana na Uhispania nusu fainali Kombe la Dunia Wanawake

Mshindi wa Jumapili atakuwa bingwa wa mpya kabisa wa Kombe la Dunia. Sweden sasa imepoteza katika nne kati ya nusu fainali tano na watacheza kutafuta nafasi ya nne au tatu.

Uhispania na Sweden walikuwa hawajahi kukutana katika Kombe la Dunia.

Bao la Carmona lilisawazishwa na Sweden katika dakika za mwisho kabla ya Uhispania kufunga bao la ushindi na kuwaduwaza wapinzani wao.

AFP