1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania yawasaka wahamiaji 48 waliozama Canary

30 Septemba 2024

Waokoaji wa Uhispania wanaendelea na juhudi za kuwatafuta wahamiaji 48 waliokuwamo ndani ya boti iliyozama karibu na visiwa vya Canary.

Wahamiaji wakiwasili kisiwa cha Canary, Uhispania.
Wahamiaji wakiwasili kisiwa cha Canary, Uhispania.Picha: Europa Press/ABACA/picture alliance

Kwa mujibu wa taarifa, mpaka sasa watu tisa wamethibitishwa kuwa wamekufa.

Ajali hiyo ilitokea wakati waokoaji hao walipokuwa wanajaribu kukikaribia chombo hicho.

Maafisa wa Uhispania wamesema matumaini ya kuwaokoa waliokuwamo ndani ya boti hiyo yamezidi kuwa finyu lakini wameeleza kuwa juhudi zinaendelea.

Soma zaidi: Watu 9 wamefariki baada ya boti yao kuzama karibu na Canary

Chombo hicho cha baharini kilichokuwa kinawasafirisha wahamiaji kilizama tangu Ijumaa usiku na miongoni mwa watu tisa waliokufa ni mtoto mmoja.

Waokoaji waliweza kuwaokoa wahamiaji  27.

Mamlaka ya Uhispania imesema wahamiaji hao wametoka Mali, Mauritania na Senegal.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW