1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uholanzi walenga kuikwepa Sweden raundi ya 16

31 Julai 2023

Mechi nyengine muhimu katika kundi G Jumanne itawapatanisha Uholanzi na Vietnam ambao washaondolewa kutoka kwenye mashindano hayo.

Neuseeland Fussball Frauen WM 2023 l USA vs Niederlande l Gruppe E l Jubel, Jill Jamie Roord
Picha: Jose Breton/NurPhoto/IMAGO

Kocha wa Uholanzi Andries Jonker anasema hawaogopi kucheza na Sweden katika mechi ya raundi ya 16 bora ila itakuwa vyema kama hawatopatana nao.

Uholanzi na Marekani wanalingana kipointi ila uholanzi wamedunishwa na uchache wa mabao.

"Hatumuogopi yeyote. Iwapo tutacheza na Sweden basi tutakwenda kwenye mechi tukiwa na lengo moja tu ila hatutowaogopa. Ila kama tunaweza kuwakwepa itakuwa vizuri ili tupatane na mpinzani ambaye si mahiri sana, kwenye karatasi tu ila tunafahamu kwamba hayo yatakuwa mapambano mengine," alisema Jonker.

Vyanzo: Reuters/DPAE/AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW