1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uholanzi yatinga robo fainali kwa kuiondoa Afrika Kusini

6 Agosti 2023

Uholanzi imetinga robo fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake na kuweka miadi na Uhispania baada ya kuhitimisha ndoto za Afrika Kusini kwa ushindi wa 2 - 0

Neuseeland Fussball Frauen WM 2023 l USA vs Niederlande l Gruppe E l Jubel, Jill Jamie Roord
Picha: Jose Breton/NurPhoto/IMAGO

Uholanzi imetinga robo fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake na kuweka miadi na Uhispania baada ya kuhitimisha ndoto za Afrika Kusini kwa ushindi wa 2 - 0. Lakini timu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili katika Kombe la Dunia la 2019 ilipitia matukio yenye tumbo joto kwenye mechi hiyo mbele ya mashabiki 40,000 mjini Sydney.

Soma pia: Kombe la dunia la wanawake: Japan yazima ndoto za Norway

Watamshukuru mlinda mlango wao kuwa kuzuia makombora ya mabingwa wa Afrika Banyana Banyana katika kipindi cha kwanza. Uholanzi itakwaruzana na Uhispania Ijumaa katika mechi ya hatua ya timu zane za mwisho itakayoikutanisha miamba ya Ulaya. 

Katika mechi inayoendelea kwa sasa, Sweden wanacheza dhidi ya Marekani. Mshindi wa mechi hiyo atakutana na Japan katika robo fainali nyingine

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW