1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru nchini Marekani wapungua,ripoti yaonyesha

Michael Kwena
19 Machi 2026

Kundi la utafiti linalounga mkono demokrasia limesema uhuru nchini Marekani umepungua hadi kiwango cha chini kabisa tangu lilipoanza tathmini yake karibu nusu karne iliyopita.

USA Boston 2025 | "No Kings" Proteste gegen Donald Trumps Politik
Kundi la Utafiti la Freedom House limebaini kuwa, hali jumla ya uhuru ilishuka kote ulimwenguni 2025Picha: Joseph Prezioso/AFP

Kundi la utafiti linalounga mkono demokrasia limesema uhuru nchini Marekani umepungua hadi kiwango cha chini kabisa tangu lilipoanza tathmini yake karibu nusu karne iliyopita, na kutaja kuwa Rais Donald Trump amekuwa akitumia vibaya na kwa mabavu mamlaka yake.

Kundi hilo kwa jina Freedom House lenye makao yake makuu Washington, limesema hali jumla ya uhuru iliporomoka kote ulimwenguni mwaka jana , hii ikiwa ni kwa mwaka wa 20 mfululizo, katika kile lilichokiita kuwa ni hatua ya kusikitisha.

Marekani bado imeorodheshwa kama nchi yenye uhuru, japo alama yake imeshuka hadi pointi 81kati ya 100,ikiwa ndiyo kiwango cha chini zaidi tangu ripoti za mwaka 1972 kuanza kutolewa. Alama hiyo inaweka Marekani kuwa sawa na Afrika Kusini, na chini ya baadhi ya washirika wake wa Ulaya pamoja na Korea Kusini na Panama.

Wasiwasi upo ndani ya vyombo vya kutunga sheria

Freedom House imeeleza kuwa kushuka kwa kiwango cha uhuru nchini Marekani kunatokana na mchanganyiko wa masuala kadhaa. Miongoni mwa masuala hayo ni migongano na kutofanyakazi vizuri kwa vyombo vya kutunga sheria, pamoja na kuongezeka kwa nguvu na ushawishi wa upande wa utendaji serikalini.

Rais wa Marekani Donald Trump Picha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Pia kumekuwepo na shinikizo kubwa dhidi ya uwezo wa watu kujieleza kwa uhuru. Aidha,ripoti hiyo inataja juhudi za utawala mpya kudhoofisha mifumo na taratibu za kupambana na ufisadi.

Kwa upande mwingine, ripoti hiyo inaeleza kwamba Rais Donald Trumpametumia vibaya mamlaka yake ya urais ikiwemo kutoa maagizo ya kufunga baadhi ya mashirika ya serikali na kuwapeleka maafisa waliojihami kupambana na wahamiaji .

Freedom House imeeleza kuwa Marekani ilipoteza pointi tatu katika tathmini ya uhuru,hii ikiwa ni kiwango kikubwa kuliko nchi nyingi. Ni nchi ya Bulgaria pekee iliyoshuka kiwango kama hicho kufuatia uchaguzi wake wa mwaka 2024 uliokumbwa na madai ya wizi wa kura.

Asilimia 21 ya watu duniani wanaoishi katika nchi huru

Kwa ujumla, shirika hilo limesema kuwa, ni takribani asilimia 21 tu ya watu duniani wanaoishi katika nchi zinazopewa hadhi ya uhuru ila mataifa mengi ya barani Afrika yamekosa kwenye orodha hiyo kutokana na mapinduzi ya kijeshi, ukatili wa waandamanaji na kudhoofika kwa uwajibikaji wa kikatiba katika mataifa mengi barani humo. Mtafiti wa Freedom House Cathryn Grothe amesema, demokrasia katika nchi nyingi imepungua. 

 

Kundi la Utafiti la Freedom House limebaini kuwa, hali jumla ya uhuru ilishuka kote ulimwenguni 2025Picha: Michael M. Santiago/AFP/Getty Images/picture alliance

Hata hivyo,licha ya kuporomoka kwa uhuru katika maeneo mengi duniani, ripoti ya Freedom House imeonyesha kuwepo kwa maendeleo chanya. Nchi za Bolivia, Malawi na Fiji zilipandishwa hadhi kutoka viwango vya mataifa yenye uhuru kiasi hadi huru kamili.

Taifa lililopata alama 100 ni Finland huku Sudan Kusini ikiwa na alama ya chini kabisa kwa kutopata alama ya 0. Aidha,Guinea Bissau ndllo taifa lililoripoti kuporomoka zaidi kwa kiwango cha uhuru ambako jeshi liliipinduwa serikali na kusimamisha mchakato wa uchaguzi siku chache baada ya zoezi la kupiga kura kuanza.

Freedom House lililoanzishwa mwaka 1941 hujiendesha kwa uhuru, lakini kihistoria imekuwa ikipokea ufadhili mkubwa kutoka kwa serikali ya Marekani. Utawala wa Rais Donald Trumphata hivyo,ulipunguza kwa kiasi kikubwa ufadhili huo kama sehemu ya hatua za kupunguza juhudi za kuendeleza demokrasia kimataifa.

  

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW