1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru wa Afrika hautosha kuwa sababu ya maendeleo

Hawa Bihoga
29 Julai 2024

Mataifa ya Afrika kupata uhuru kuliibua hisia kote barani humo lakini lilipokuja suala la maendeleo na kustawisha uchumi wa mataifa hayo, uhuru pekee unatajwa kuwa hautoshi kufikia malengo katika nchi yoyote barani humo.

Afrika | Bendera za mataifa
Mwanmke akiwa katikakati ya bendera za mataifa ya AfrikaPicha: SIPHIWE SIBEKO/REUTERS

Nyaraka za kihistoria zinaonesha kwamba katika miaka 1950, Liberia na Ethiopia ndizo nchi mbili pekee za Kiafrika ambazo hazikutawaliwa na wakoloni.

Lakini hivi sasa karibu mataifa yote barani humo yanao uhuru wao ikiwemo Sudan Kusini, Eritrea na Namibia, miongoni mwa mataifa mengine.

Hata hivyo taswira ya uhuru inatafsiriwa tofauti na wataalamu mbalimbali wa masuala ya uongozi na usalama, profesa Juste Codjo ambae ni mchambuzi wa masuala ya usalama kutoka Benin aliiambia DW kwamba licha ya mataifa ya Afrika kupata uhuru wake, lakini hakuna uthibitisho kwamba mataifa hayo yana uhuru kikamilifu.

Soma pia:Jeshi la Nigeria laonya vijana juu ya maandamano ya vurugu kama yaliyofanyika Kenya

Hoja hiyo inatiwa uzito na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka nchini Ghana Fidel Amakye Owusu akisema taswira kamili ya uhuru inategemea taifa moja hadi jingine akitolea mfano taifa kama vile Namibia ambalo linaonekana kuwa na mafanikio makubwa zaidi ukilinganisha na Sudan Kusini licha ya mataifa yote mawili kuchukua mwelekeo sawa katika kupata uhuru wake.

Aliongeza kwamba aina ya uhuru kwa mataifa ya Afrika ambayo yalipata ulitegemea kwa kiwango kikubwa nguvu ya kikoloni ambayo ilikuwa inatawala nchi husika.

Sudan Kusini katika mfano wa hoja hii

Katika kauli hii hebu tuliangalie taifa la Sudan Kusini, taifa hili lilisherehekea miaka 13 ya uhuru mnamo Julai 9.

Hata hivyo katika muda huo mfupi, nchi hiyo imelazimika kustahimili vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka saba. Mnamo 2017, Umoja wa Mataifa ulitangaza njaa kote nchini humo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akionesha Katiba mpya ya taifa hiloPicha: Andrew Burton/picture alliance/AP

Zaidi ya hayo taifa hilo linakabiliwa na mizozo ya kisiasa kwa miaka mingi ukiweka mbali changamoto za majanga ya asili ambayo yanaripotiwa nchini humo.

Msomi wa maendeleo ya kimataifa wa Sudan Kusini James Boboya aliiambia DW kwamba awali, kulikuwa na matumaini makubwa nchini humo.

Soma pia:Marekani yaandaa mazungumzo ya kusitisha mapigano Sudan

Walakini, mambo yalibadilika kwa haraka akisema watumishi wa umma ikiwemo wanajeshi wanakaa kwa takriban miezi 8 hawajalipwa mishahara yao akiongeza kwamba serikali iliopo ilichokirithi kutoka Sudan ni migogoro, rushwa, ukosefu wa huduma pamoja na usimamizi mbaya wa rasilimali, akisisitiza kwamba haya yote yamesababisha kutengwa, ukosefu wa uhuru pamoja na maendeleo.

Wachambuzi pia wanakubaliana kwamba kuna jambo moja lisiloonekana la uongozi, ambalo linatazamwa kama kurithi matatizo ya kihistoria ambayo kwa hakika linaweza kupinga taifa lolote jipya ambalo ni huru.

Uongozi ni chachu kufikia malengo ya Afrika

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa nchini Ghana Owusu anasema kwamba uongozi wa kisiasa baada ya uhuru ulikkuwa ni kama upanga wenye ncha kaliukiwa na viongozi wenye maono kama Nelson Mandela, Julius Nyerere na Kwame Nkrumah wakiwa na mchango mkubwa katika kukuza umoja wa kitaifa, maendeleo ya kijamii na maendeleo ya kiuchumi.

Kwa upande mwingine wachambuzi hao wanaamini kwamba uongozi mbovu wenye sifa ya rushwa, upendeleo na ubabe umechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kwa mataifa mengi ya Afrika.

Umma unasemaje kuhusu safari za viongozi nje ya nchi?

02:42

This browser does not support the video element.

Msomi wa Sudan Kusini Boboya ana maoni sawa kuhusu uongozi katika muktadha wa nchi yake, akisema kumekuwa na wababe wengi wa kivita na viongozi wa kisiasa ambao walichukua mamlaka na walianza kuhimiza uasi kote Sudan Kusini hatua ambayo imelisababisha taifa hilo kuelekea kwenye "mmomonyoko."

Soma pia:WHO yaonya juu ya kuongezeka kwa mashambulizi kwenye hospitali nchini Sudan

Baadhi ya Waafrika, hata hivyo, wanaamini kuwa ni wakati wa kuondoka kwenye kivuli cha ukoloni na kuangalia uhalisia wa mafanikio ndani ya Afrika.

Owusu analiangalia hilo kwa mfano Rwanda hasa katika kuhamasisha mataifa mengine ya Afrika, akisema taifa hilo dogo la Afrika Mashariki limethibitisha kwamba nchi inaweza kusonga mbele kutoka katika hali mbaya kama vile mauaji ya kimbari ya 1994 lililoshuhudia taifa hilo hadi kuleta utulivu na maendeleo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW