Uhuru wa vyombo vya habari Burundi
1 Mei 2007Ikiwa ni nchi iliotokana na miaka 10 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, Burundi sasa imo katika utaratibu wa demokrasia na amani. Pamoja na hayo mapigano huripotiwa hapa na pale, lakini hali inaanza kuboreka baada ya uchaguzi uliotajwa kuwa huru na wa haki.
Pamoja na hayo sheria bado haiajashika mizizi. Kumekuweko na visa vya watu kukamatwa hovyo na hata taarifa za mateso na ukandamizaji wa uhuru wa kutoa maoni, licha ya kwamba vyombo huru vya habari vinaruhusiwa kisheria, lakini mkono wa serikali bado unatumika. Jaribio la mapinduzi mwezi Agosti ni tukio lililoifanya hali kuwa hata mbaya zaidi.
Sheria ya vyombo vya habari ya 1977 bado inatumika, ikipiga marufuku utoaji habari zinazoonekana kuwa ni za uchochezi au kusababisha kuvurugika kwa amani miongoni mwa raia .
Sheria zaidi inayohusiana na vyombo vya habari ya 2003, inataja juu ya utozaji faini na kifungo jela cha hadi miaka mitano kwa kosa la upotoshaji habari zinazohusu dola au mtu binafsi, au zinazo mtusi Rais wan chi. Ama hatua ya maendeleo katika sheria hiyo, ni kuondolewa kifungo kinachotaka magazeti yawasilishe makala kwa ukaguzi kabla ya kuchapishwa.
Mwaka 2006-Agosti, kuliripotiwa ukiukaji wa uhuru wa vyombo vya habarii na serikali ikaanzisha kampeni ya kuwaandama waandishi habari kadhaa walioripoti juu ya jaribio lililodaiwa kuwa la mapinduzi.
Aprili 17 mwaka jana, kiasi ya waandishi habari 20 walizuiwa mateka na polisi baada ya kukusanyika kuhudhuria mkutano wa wana habari ulioitishwa na mbunge Mathias Basabose, ambapo alitaka kuelezea juu ya mkasa wa kufukuzwa kwake katika chama tawala CNDD-FDD.
Mei 31 serikali ikamtia ndani mwandishi habari Aloys Kabura, kwa kosa la kutoa maoni yake akiwa katika baa moja ambayo mwanasheria wa serikali Jean Paul Manwagari aliyataja kuwa ni ya kuipaka matope serikali. Kabla ya hapo Kabura alikua ameandika makala akiihusisha polisi katika biashara ya magendo. Kabura aliachiwa huru Oktoba 30 baada ya kuwa jela miezi mitano.
Agosti 3, muanzilishi na mkurugenzi wa Redio ya umma ambayo ni ya bninafsi RPA, Alex Sinduhije, alikimbilia mafichoni akihofia kukamatwa. Alihusisha na ripoti za jaribio la mapinduzi. Serikali pia iliwatia nguvuni wanasiasa kadhaa kuhusika na jaribio hilo akiwemo rais wa zamani .
Tarehe 12 Septemba barua iisiyo na jina wala sahihi ilitumwa katika Radio Isangiro kuisdhutumu kwa kuipaka matope serikali. Risala ilikua “ Fungeni au tutawalazimisha mfunge redio yenu.”
Risala hiyo iliandamana na vitisho vya kuuwawa waandishi wa redio hiyo na familia zao. Siku hiyo hiyo, kundi la watu likamvamia mwaandishi habari wa Isangiro, tatien Nkeshimana alipotoka kuripoti hotuba ya Rais Nkurunziza. Watu hao wakapora, zana zake za kazi na simu yake ya mkononi.
Hiyo ndiyo ripoti ya taasisi ya kimataifa ya vyombo vya habari 2007, kuhusu uhuru wa vyombo vya habari Burundi 2006, siku inayoadhimishwa kimataifa kesho Mei 3.
Ripoti ya taasisi hiyo ya kimataifa inasema pamoja na yote kuna dalili kwamba hali inazidi kuwa ya uwazi zaidi na kuongezeka kwa kiwango cha uhuru wa vyombo vya habari nchini Burundi.