Uhusiano wa Sudan na Ethiopia wayumba
29 Juni 2022Wanajeshi wa Sudan wamefyatua silaha nzito wakati wa makabiliano katika eneo la mashariki lilalozozaniwa ambalo linapakana na Ethiopia, kwa mujibu wa afisa wa Ethiopia, likiwa tukio la karibuni zaidi katika mzozo wa muda mrefu kuhusu mpaka wao wa pamoja.
soma Bwawa kubwa la utata la Ethiopia
Afisa wa jeshi la Sudan ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa sababu hana ruhusa ya kuzungumza na vyombo vya habari amesema Sudan jana ilifanikiwa kulikamata eneo la Jabal Kala al-Laban, lililo karibu na mpaka huo unaogombaniwa kufuatia mashambulizi ya mizinga na ndege.
soma Misri, Sudan zasitisha mazungumzo na Ethiopia
Assefa Ashege, afisa mwandamizi wa usalama katika jimbo la Amhara la Ethiopia amesema jeshi la Sudan lilifyatua mizinga ya masafa marefu kuanzia Jumatatu asubuhi hadi jana mchana, lakini hakuna aliyeumia.
Ethiopia ilikanusha Jumatatu tuhuma za Sudan kuwa jeshi lake liliwakamata na kuwauwa wanajeshi saba wa Sudan na raia mmoja, na badala yake kusema mauaji hayo yalifanywa na wanamgambo wa eneo hilo.