1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhusiano wa Ujerumani na Afrika 'siyo kampeni ya hisani'

19 Julai 2024

Ujerumani inaondoa wanajeshi wake kutoka kanda ya Sahel inayokumbwa na ugaidi, huku inataka kupanua uhusiano na mataifa ya kanda ya Afrika Magharibi kwa sababu usalama wa Umoja wa Ulaya unaitegemea kanda hiyo.

Dakar, Senegal | Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock akizungumza wakati wa ziara yake nchini Senegal.Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Mitaa ya mji mjuu awa Senegal Dakar inabadilika. Bado imejaa magari mengi, pikipiki na hata magari ya kukokotwa na farasi, ambayo mara nyingi hukwama kwenye msongamano wa magari.

Lakini kaskazini mwa jiji hilo la watu milioni nne, katika wilaya ya Parcelles Assainies yenye maendeleo duni ya kijamii, mapinduzi ya trafiki yanatokea.

Miezi mitatu tu iliyopita, iliwachukua wakazi saa moja na nusu kufika kazini au shuleni katikati mwa jiji. Sasa, ni nusu tu ya muda huo. Njia mpya ya mabasi ya umeme huruka msongamano wa magari na kuwafikisha Wasenegali kwenye vituo vyao haraka.

Mfumo wa mabasi ya kasi umeifanya Dakar kuwa kinara wa usafiri wa kisasa wa mijini barani Afrika. Mabasi hayo yanatoka China, lakini vitengo vya udhibiti vinavyotumia teknolojia ya kisasa vinatoka kampuni ya Kijerumani ya CarMedialab, inayotekeleza mifumo ya uchukuzi inayotumia nishati mbadala duniani kote.

Soma pia:Baerbock atazama mazoezi ya kupambana na ugaidi Ivory Coast

Henri Depe Tschatchu, meneja mtendaji wa CarMedialab, aliandamana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock katika safari yake ya karibuni zaidi Afrika Magharibi.

Na ingawa bara hilo siyo rahisi kwa uchumi wa Ujerumani kupenya, linatoa soko la uhakika kwa siku zijazo. Baada ya Dakar, kampuni hiyo inataka kujitanua hadi Kenya, Nigeria na Ivory Coast, Tschatchu aliiambia DW.

Senegal: Mwanga wa matumaini

Ziara ya Baerbock ilikuja muda mfupi baada ya Senegal kufanikisha mabadiliko kiutawala  ya kidemokrasia. Aliandamana na ujumbe wa wafanyabiashara 10. Safari hiyo ililenga kutafuta fursa zaidi za uwekezaji Afrika Magharibi, ili kuchangia katika kuleta utulivu wa eneo hilo.

Wakati viongozi wa mapinduzi ya kijeshi wanatawala katika Sahel na ugaidi ukiendelea kuongezeka, nchi kama Senegal na Ivory Coast, zinaonekana kama nguzo za utulivu katika eneo hilo.

"Senegal imeanzisha mabadiliko ya kisiasa ndani ya mfumo wa kidemokrasia," Baerbock alisema.

Kwa takriban siku 100, Senegal imekuwa ikiongozwa na wanachama wawili wa zamani wa upinzani ambao hadi hivi karibuni walikuwa wafungwa wa kisiasa: Rais Bassirou Diomaye Faye na Waziri Mkuu Ousmane Sonko.

Chama chao cha Patriots of Senegal for Work, Ethics and Fraternity (PASTEF) kinasimamia kurejea kwa maadili ya kitaifa na kuachana na enzi na mila za ukoloni. Faye na Sonko wanataka kujenga Senegal inayojiamulia na kujiamini. Na, wanatafuta wawekezaji.

 

Usalama wa EU unaitegemea Afrika

Nguvu kuu ya Senegal ni vijana wake wenye ari ya kufanya kazi. Lakini wanakosa elimu ya msingi na ajira.

Baerbock alisema Ujerumani inataka kuwatendea washirika wake wa Afrika kwa usawa, hii kimaanisha kuiwezesha miradi ya bara hilo kupata mikopo nafuu na ufadhili.

Ufafanuzi:Kwanini Niger ni muhimu kwa mataifa ya magharibi?

01:26

This browser does not support the video element.

Baerbock alibainisha kuwa kwa sasa wadau wa Afrika wanapokea masharti mabaya zaidi kuliko wenzao wa Ulaya, alibainisha Baerbock.

"Hii si kampeni ya hisani, bali kwa maslahi yetu wenyewe ya usalama," Baerbock alisema. "Popote ambapo sisi kama demokrasia na Ulaya hatuwekezi, wengine huwekeza, na kujenga utegemezi ambao, yanapotokea mashaka, unatumiwa dhidi yetu na maslahi yetu ya usalama."

Soma pia:Baerbock afanya ziara Ivory Coast baada ya Senegal

Katika kanda hiyo, ushawishi wa China, Urusi na Uturuki unakuwa kwa kasi kubwa. Baerbock alisema mataifa ya pwani ya Afrika Magharibi yalikuwa yanazingatgiwa kwa sasa kuwa salama na tulivu.

Lakini endapo ukuaji wa uchumi wa Senegal utadorora na ukataji tamaa kuongezeka, hali inaweza kubadilika.

Ikiwa vijana hawana matarajio, wataandikishwa kwa urahisi zaidi na magenge ya wahalifu na magaidi au kuondoka katika nchi zao, alisema, jambo ambalo lingepeleka watu wengi zaidi waliokimbia makazi yao kuelekea Ulaya. "Usalama na fursa za siku zijazo za eneo hili zinahusishwa kwa karibu na usalama wa Ujerumani."

Usalama bado ni suala kuu

Baerbock ilipotua Abidjan, Ivory Coast, waandishi wa habari walitaka kujua kwa nini Ujerumani inajiondoa kabisa kutoka Niger na inawekeza wapi katika usalama wa Afrika.

Baerbock alisema kujiondoa huko kutaathiri tu uwepo wa jeshi la Ujerumani, lakini ufadhili wa maendeleo unaendelea kumiminika kwa sababu watu ambao wanateseka na ugaidi hawahusiki na hali hiyo.

Uamuzi wa serikali ya Ujerumanikuwaondoa wanajeshi wake kutoka Niger ifikapo mwisho wa Agosti unaweza kumaanisha kuwa Wasaheli wamewaachwa kabisaa kwa viongozi wa mapinduzi ya kijeshi na mamluki wa Urusi.

Ujerumani yaunga mkono mapambano ya Ivory Coast dhidi ya ugaidi

Ikilinganishwa na Sahel, Pwani ya Afrika Magharibi ni tulivu. Lakini utulivu huo utadumu kwa muda gani? Rais wa Ivory Coast Allasane Outtara anasema nchi hiyo ni tulivu na itaendelea kuwa hivyo kwa sababu imewekeza vilivyo na inaliamini jeshi la jamhuri la Ivory Coast.

Ujerumani yaahidi kuongeza ushirikiano wa kijeshi na Niger

02:36

This browser does not support the video element.

"Ninaweza kukuhakikishia kuwa Ivory Coast ni nchi tulivu na itabaki kuwa hivyo," Rais wa Ivory Coast Alassane Quattara alisema mjini Abidjan. Serikali imewekeza sana na anaamini "jeshi la ulinzi wa Jamhuri la Ivory Coast."

Bila shaka Ivory Coast imejiandaa kwa mzozo. Siyo mbali na Abidjan, kuna kituo kikubwa zaidi cha mafunzo ya kupambana na magaidi. Ujerumani inasaidia kituo hicho kwa kiasi cha euro milioni 2.5 kila mwaka.

Soma pia:Baerbock afanya ziara Afrika Magharibi

Baerbock alitazama mazoezi kwa karibu. Katika "Operesheni Trampoline," kijiji cha kubuni kinachodhibitiwa na magaidi kinakombolewa na vikosi maalum vya jeshi la Ivory Coast.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani alimuuliza kamanda ni mara ngapi uvamizi na operesheni kama hizo hufanyika. Hakuweza kutoa takwimu maalum, lakini nakuhakikishia Baerbock, hutokea mara kadhaa kwa mwaka.

Huku Ivory Coast ikipambana na mwenendo wa mapinduzi yanayoyumbisha kanda hiyo, Ujerumani itakuwa na nafasi ya kutoa mchango muhimu katika mustakabali wa Afrika Magharibi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW