1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhusiano wa Ujerumani na Poland waingia enzi mpya

7 Desemba 2007

BERLIN

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani anaamini kwamba uhusiano kati ya serikali yaUjerumani na serikali ya Poland umeingia enzi mpya.

Frank Walter- Steinmeir alikutana na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Poland Radoslav Sikorski mjini Berlin hapo jana kwa mazungumzo ambayo Steinmeir amesema yanaweza kuanzisha tena mikutano ya kawaida kati ya serikali za nchi hizo mbili.

Uhusiano kati ya nchi mbili hizi jirani umeathirika katika miaka ya hivi karibuni lakini umeanza kuboreka chini ya Waziri Mkuu mpya wa Poland Donald Tusk.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW