SiasaMarekani
Uhusiano wa Ulaya na China kupimwa kwa tabia za China
16 Aprili 2023Matangazo
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema mapema leo katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa mashauriano wa mawaziri wa mamnbo ya kigeni wa kundi la G7 nchini Japan, akiangazia masuala hayo mawili miongoni mwa yatakayopewa kipaumbele kabla ya kuanza rasmi kwa mkutano huo wa siku tatu.
Borrell amesema chochote kitakachotokea katika Ujia wa Bahari wa Taiwan kitakuwa na umuhimu mkubwa kwao, na kusisitiza umuhimu wa kuihusisha na kuwa na mawasiliano ya wazi na China aliyoielezea kama mshirika, mshindani na mpinzani wa kimakakati.
Mawaziri hao wanatarajiwa kujadiliana juu ya mtizamo wa pamoja kuelekea China, hii ikiwa ni kulingana na afisa wa wizara ya mambo ya kigeni wa Marekani.