1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUlaya

Uingereza kuanzisha mazungumzo ya kibiashara na Korea Kusini

21 Novemba 2023

Uingereza na Korea Kusini zitaanzisha mazungumzo juu ya mkataba wa biashara huria na kutia saini makubaliano ya kidiplomasia wakati wa ziara ya kiserikali ya rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol nchini Uingereza wiki hii.

Mkutano wa ASEAN mjini Jakarta
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk YeolPicha: Tatan Syuflana/AP Photo/picture alliance

Mkataba huo mpya wa biashara huria utachukua nafasi ya mkataba uliopo sasa ambao kwa kiasi kikubwa, una vipengee vilivyokuwepo hata kabla ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

Ziara ya Yoon inaanza rasmi leo ambapo atakaribishwa na Mfalme Charles, kwa kupewa heshima kuu za kijeshi na kuandaliwa karamu katika kasri la Buckhingham, kuashiria ziara ya kwanza ya serikali iliyoandaliwa na Uingereza tangu kutawazwa Charles kuwa mfalme.

Yoon, mhafidhina ambaye ametaja changamoto nyingi za kimataifa kama sababu ya kutafuta uhusiano wa karibu na washirika wenye fikra sawa , pia atahutubia mabunge yote mawili ya Uingereza, kabla ya kufanya mazungumzo na Sunak juu ya biashara, teknolojia na ulinzi.

Kupitia taarifa Sunak ameeleza kuwa, makubaliano kati ya Uingereza na Korea Kusini yatachochea uwekezaji, kukuza biashara na kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.