1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel

16 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, amesema kuwa nchi hiyo inafikiria kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel, hatua inayoongeza shinikizo kwa serikali ya Tel Aviv juu ya hatua zake huko Mashariki ya Kati.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir StarmerPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Vikwazo hivyo vitawahusu Waziri wa Fedha, Bezaleli Smotrich na Waziri wa Usalama, Itamar Ben-Gvir ambao wanahusishwa na hatua za kuzuia misaada kuingia katika Ukanda wa Gaza na kutanua makazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Alipokuwa akihojiwa na Bunge la Uingereza, Starmer amesema mawaziri hao walitoa ''maoni ya kuchukiza" juu ya hali katika maeneo hayo ambayo kwa Gaza pekee idadi ya vifo imepindukia watu 42,000 huku kukiwa na ugumu wa upatikanaji wa huduma za msingi.