Uingereza na Rwanda mahakamani juu ya mkataba wa wahamiaji
18 Machi 2026
Matangazo
Maafisa kutoka nchi hizo mbili watawasilisha kesi yao katika kikao cha siku tatu mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 1899 kusuluhisha mizozo ya kimkataba kati ya mataifa.
Maafisa kutoka Rwanda watawasilisha kesi yao leo Jumatano, huku mawakili wa Uingereza wakijibu kesho Alhamisi. Pande zote mbili zitahitimisha uwasilishaji wao siku ya Ijumaa.
Jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ya PCA litasimamia kesi hiyo na huenda likachukuwa miezi kadhaa kutoa uamuzi.
Tayari mataifa hayo mawili yako kwenye mvutano baada ya Uingereza kupunguza misaada kwa Rwanda, ikiituhumu kuwaunga mkono waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.