1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza na Ujerumani kushirikiana zaidi katika ulinzi

25 Julai 2024

Ujerumani na Uingereza zimeahidi kushirikiana kwa karibu zaidi katika sekta ya ulinzi na usalama kama sehemu ya serikali mpya ya chama cha Leba.

Rekruten bei der Bundeswehr | Recruits at the Bundeswehr
Picha: Thomas Koehler/photothek/picture alliance

Hii ni kwa ajili ya kurejesha mahusiano na washirika wa Ulaya baada ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

Katika ziara yake ya kwanza mjini Berlin, waziri wa ulinzi wa Uingereza John Healey ametia saini makubaliano na mwenzake Boris Pistorius ambayo yamesifiwa kuwa ya aina yake kati ya washirika hao wa jumuiya ya kujihami ya NATO.

Makubaliano hayo yanajumuisha kando na mambo mengine, ahadi ya kuimarisha sekta ya ulinzi katika nchi zote mbili, ushirikiano katika maendeleo na ununuzi wa silaha na kuratibu njia bora za kuisaidia Ukraine.

Pistorius amewaambia waandishi wa habari kuwa, makubaliano hayo yataimarisha pia nguzo ya Ulaya ndani ya jumuiya ya NATO.

Makubaliano hayo yanatokea wakati serikali mpya ya Uingereza, baada ya ushindi wa kishindo mwezi huu, inapojaribu kurejesha uhusiano wake na Ulaya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW