Uingereza yahofia mashambulizi ya kigaidi ziara ya Biden
28 Machi 2023Matangazo
Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kuhudhuria kumbukumbu ya miaka 25 tangu yalipofikiwa makubaliano ya amani ya kihistoria, Aprili 10 mwaka 1998 yanayotambuliwa kama "Makubaliano ya Ijumaa Kuu", ambayo yalimaliza machafuko ya umwagaji damu Ireland Kaskazini.
Kwa mujibu wa kiongozi mkuu wa Ireland Kaskazini, Chris Heaton-Harris, Shirika la Ujasusi la Uingereza (MI5), linaamini kitisho cha kutokea mashambulizi ni kikubwa.
Ametowa mwito kwa umma wa Ireland Kaskazini kuwa makini lakini pia kutotaharuki kufuatia tangazo hilo.