1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yaiadhibu Urusi,kutumia silaha za kemikali Ukraine

8 Oktoba 2024

Serikali ya Uingereza imekichukulia hatua kitengo cha kemikali na kibaolojia cha wanajeshi wa Urusi pamoja na kamanda wake, Igor Kirillov, kwa madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Ukraine.

Ukraine | Russischer Luftangriff auf Cherson
Hali ilivyo baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya angani kwenye maeneo ya makazi na taasisi ya elimu huko Kherson, Oktoba 07, 2024.Picha: Kherson Regional Military Administration/Anadolu/picture alliance

Uingereza na Marekani zinaishutumu Urusi kwa kutumia sumu aina ya chloropicrin dhidi ya wanajeshi wa Ukrainekinyume na Mkataba wa Silaha za Kemikali (CWC). Urusi imekanusha tuhuma hizo na kusema haimiliki tena aina hiyo ya silaha za kemikali.Chloropicrin ni kioevu chenye mafuta na harufu kali chenye uwezo wa kuua kwa kuziba pumzi na ambacho kilitumiwa sana wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia kama aina ya bomu la kutoa  machozi.