1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kuisaidia Kongo katika jitihada za kudhibiti mpox

22 Agosti 2024

Serikali ya Uingereza imeiahidi Kongo kitita cha pauni milioni 3.1 kwa ajili ya kusaidia kupambana na mripuko wa homa ya Mpox ambao tayari umeshauwa watu zaidi ya 500 na kuathiri wengine kadhaa.

Kipimo cha homa ya Mpox kikionesha maambukizi.
Kipimo cha homa ya Mpox kikionesha maambukizi.Picha: Dado Ruvic/Illustration/REUTERS

Serikali ya Uingereza imeiahidi Kongo kitita cha pauni milioni 3.1 kwa ajili ya kusaidia kupambana na mripuko wa homa ya Mpox.

Akizungumza baada ya kuitembelea Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba ya Kibayolojia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya Afrika Ray Collins ametoa ahadi ya fedha hizo jana Jumatano ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo, ambao awali ulifahamika kama homa ya nyani.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani - WHO, karibu visa 15,000 vya mpox vimegundulika nchini Kongo katika mwaka wa 2024, huku kukiwa na vifo 500.

WHO pia imegundua zaidi ya visa 20,770 vya kipindupindu nchini Kongo katika miezi saba ya kwanza ya mwaka wa 2024, huku kukiwa na miripuko ya kiwango sawa na hicho nchini Ethiopia, Zambia na Zimbabwe.

Soma pia:Ujerumani kusaidia kubaini visa vya Mpox nchini Kongo

Collins amesema ziarani Kinshasa kuwa Uingereza inashirikiana na washirika na kwa kutumia wanasayansi wakiwemo wa nchini Kongo ili kuhakikisha kuwa na mchango muhimu katika kuhakikisha usalama wa afya duniani kote. 

Wakati huo huo, Serikali ya Ujerumani imesema itapeleka Kongo maabara ya kuhamishika ili kusaidia kuwagundua wagonjwa wa homa ya Mpox na kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo imesema pia kuna mipango ya kutoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ili waweze kutambua dalili na kuufahamisha umma kuhusu hatua za kuzuia ugonjwa huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW