1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yakabilliwa na mgomo mkubwa wa sekta ya umma

1 Februari 2023

Uingereza inatarajiwa kuathiriwa na mgomo mkubwa leo wa hadi wafanyakazi nusu milioni wakiwemo walimu, wafanyakazi wa umma, madereva wa treni na wahadhiri wa vyuo vikuu nchini humo.

Großbritannien Streik
Picha: Kin Cheung/AP Photo/picture alliance

Shule zitafungwa, hakutakuwa na huduma za treni katika sehemu nyingi ya nchi hiyo, na maafisa wa jeshi wamewekwa ange kusaidia kushika doria kwenye mipaka ya nchi.

Kutakuwa pia na maandamano dhidi ya sheria mpya inayopangwa ya kuzuia migomo katika baadhi ya sekta.

Vyama vya wafanyakazi vimesema pendekezo hilo litaharibu uhusiano zaidi.

Serikali imesema mgomo huo ambao ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwa miaka mingi, utavuruga shughuli nyingi kote nchini humo.

Wiki ijayo, wauguzi, wafanyakazi wa huduma za dharura na wengine wa sekta ya afya pia wanatarajia kugoma.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW