1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yakusudia kupunguza gesi chafu kwa asilimia 81

12 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ametangaza kuwa nchi yake inakusudia kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kwa asilimia 81 katika viwango vya miaka ya 90, ifikapo 2035.

Keir Starmer
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza Keir Starmer Picha: Benjamin Cremel/AP/picture alliance

Starmer amebainisha malengo hayo mapya katika mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira wa COP29 unaofanyika Baku nchini Azerbaijan.

"Lengo letu la nyuzi joto 1.5 linalingana na malengo yetu ya ukuaji. Lakini tatizo hili pia linahitaji ushirikiano wa kimataifa, na ndiyo maana tumechukua fursa katika mkutano huu wa COP kuzihimiza  pande zote kujitokeza na malengo yao kabambe," alisema Starmer.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza ndiye kiongozi pekee wa kundi la nchi zilizostawi kiuchumi la G20 aliyejitokeza katika mkutano huo.