1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yaongeza kasi kuelekea wasi wasi kuhusu Brexit

Sekione Kitojo
21 Februari 2019

Wabunge wa Uingereza wanaweza kupata fursa ya kuyapigia kura mabadiliko ya makubaliano ya Brexit wiki ijayo wakati wajumbe wa majadiliano mjini Brussels wanahangaika kupata mabadiliko ya dakika za mwisho ya mkataba. 

Belgien May trifft Juncker auf Suche nach Brexit-Durchbruch in Brüssel
Picha: Getty Images/T. Monasse

Hadi  pale  waziri  mkuu Theresa  May  atakapoweza  kupata makubaliano  ya  Brexit  yatakayoidhinishwa  na  bunge  la Uingereza, hapo  ndio atakapoweza  kuamua  iwapo kuchelewesha Brexit  ama  aliingize  taifa  hilo  lenye  uchumi  wa  tano  mkubwa duniani  katika  mkanganyiko  kwa  kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya bila  ya  makubaliano  hapo  Machi 29.

Theresa May , waziri mkuu wa UingerezaPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Parsons

Waziri  mkuu  Theresa  May  hata  hivyo  amesema  amepiga  hatua katika  mazungumzo  na  Umoja  wa  Ulaya  jana  wakati  akitafuta kupata  madhiriano  zaidi  katika  masharti ya Uingereza  kujitoa, lakini kama  ilivyotarajiwa  hakukuwa  na  mafanikio  makubwa.

"Nilikuwa  na  mkutano  mzuri  na  rais Juncker jioni hii. Nilisisitiza haja  ya kuona  mabadiliko yenye uwezo  wa mabadiliko  ya kisheria katika suala  la  mpaka kuhakikisha kwamba  hautakuwa  wa  milele. hicho  ndio  kinachohitajika iwapo  makubaliano  yatapita  katika  baraza  la  wawakilishi. Tumekubaliana  kwamba  kazi  ya  kutafuta  suluhisho itafanyika  haraka."

Alipoulizwa  kitu  gani  kitatokea  wiki  ijayo, waziri  wa  fedha  Philip Hammond  alisema  kwamba  huenda  kutakuwa  na  fursa  ya kulipigia  kura  suala  hilo  bungeni, kunaweza  kuwa  na  fursa, lakini hilo litaweza  kutokea  kwa  kutegemea  hatua  za  maendeleo ambazo  zitafikiwa  katika  siku  chache  zijazo.

Waziri wa fedha wa Uingereza Philip HammondPicha: Getty Images/AFP/N. Halle'n

Hofu inaongezeka

May , ambaye  mwanzo  alikuwa akisita sita  kuunga  mkono uanachama  wa  Umoja  wa  Ulaya  ambaye  alifanikiwa  kuchukua uongozi  huo  wa  juu  katika  mtafaruku  wa  kisiasa  kufuatia  kura ya  maoni  mwaka  2016, aliahidi  kuwapa  wabunge  fursa  ya kuamua  kile  kinachotakiwa  kufanyika  juu  ya  Brexit hapo  Februar 27, hadi  pale  atakapoweza  kurejesha  tena  makubaliano hayo.

Hofu inaongezeka  kwamba  Uingereza  inaweza  kujitoa  bila  ya makubaliano, na  kumekuwa  na hali  nyingine  ya  mtafaruku  kabla ya  may  kwenda  Brussels  wakati  wabunge  wake  watatu walipojiuzulu  kutoka  chama  cha  Conservative wakipinga  kuhusu Brexit  na  kujiunga  na  kundi  jipya  huru  la  wabunge.

Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude JunckerPicha: picture-alliance/dpa/S. Gollnow

May amesema  waziri  wake  wa  Brexit Stephen Barclay  na mwanasheria  mkuu  Geoffrey Cox watakwenda  Brussels leo , siku tatu  tu  tangu  walipofanya ziara  ya  mwisho, wakati  kasi  ya majadilino  ikiongezeka.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri:Yusuf Saumu

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW