1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza yasaini kandarasi ya mradi wa nyambizi mpya

2 Oktoba 2023

Uingereza imetia saini kandarasi yenye thamani ya dola bilioni 4.8 kufadhili awamu mpya ya mradi wa nyambizi za kisasa zaidi wa SSN-AUKUS.

USA | AUKUS Treffen
Picha: Stefan Rousseau/AP Photo/picture alliance

Mikataba iliyosainiwa inahusisha makampuni ya Uingereza ya BAE Systems, Rolls-Royce na Babcock na ni sehemu ya muungano wa kijeshi wa Marekani, Australia na Uingereza ufahamikao kama AUKUS.

Muungano huo una lengo la kukabiliana na nguvu za kijeshi za China katika eneo la Asia-Pasifiki

Viongozi wa AUKUS walizindua mradi huo wa pamoja mwezi Machi mwaka jana katika makubaliano ambayo yatapelekea Australia kuziba pengo la nyambizi zake zinazotumia dizeli na zile zinazotumia nguvu za nyuklia ambazo zina uwezo mkubwa zaidi.

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya kijeshi ya Uingereza imesema uwekezaji huo utahusisha pia kazi ya uendelezaji hadi 2028 na kuajiri zaidi ya watu 5,000 katika eneo lake la Barrow-in-Furness kaskazini mwa Uingereza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW