1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUingereza

Uingereza yasisitiza kuwapeleka baadhi ya wahamiaji Rwanda

16 Novemba 2023

Serikali ya Uingereza imesema bado itaendelea kujaribu kuwapeleka baadhi ya wahamiaji nchini Rwanda licha ya mahakama ya juu ya nchi hiyo kutoa uamuzi dhidi ya mpango huo wa serikali

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akizungumza wakati wa mkutano na waziri mkuu wa Sweden katika ofisi yake ya Downing Street mjini London mnamo Juni 19, 2023
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi SunakPicha: Kin Cheung/REUTERS

Waziri mkuu wa Uoingereza Rishi Sunak, ambaye ameahidi kuwazuia wahamiaji kufika Uingereza kwa kutumia maboti madogo kupitia ujia wa bahari wa Uingereza, amesema  uamuzi huo haukuwa matokeo waliyoyataka lakini akaapa kuendelea na mpango huo na kutuma ndege za kwanza za kuwasafirisha wahamiaji hao kuelekea Rwanda kufikia msimu ujao wa masika.

Soma pia:Mahakama ya Juu Uingereza yasema mpango wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda ni kinyume cha sheria

Sunak amesema mahakama imethibitisha kuwa kanuni ya kuwahamisha waomba hifadhi kwa taifa la tatu ni halali hata kama iliamua kuwa Rwanda sio salama.

Sunak atishia kujiondoa katika mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu

Sunak amependekeza kuwa ikiwa changamoto za kisheria kwenye mpango huo zitaendelea, yuko tayari kuzingatia kujiondoa katika mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, hatua ambayo huenda ikaleta upinzani mkali na ukosoaji wa kimataifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW