1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroRwanda

Uingereza yasema inajiandaa kuiwekea Rwanda vikwazo

25 Februari 2025

Rwanda kuwekewa vikwazo na Uingereza kutokana na dhima ya nchi hiyo kwenye machafuko yanaendelea taifa jirani la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Uingereza yasema inajiandaa kuiwekea Rwanda vikwazo
Uingereza yasema inajiandaa kuiwekea Rwanda vikwazo Picha: GUILLEM SARTORIO/AFP/Getty Images

Uingereza imesema itatangaza vikwazo dhidi ya Rwanda kutokana na dhima ya nchi hiyo kwenye machafuko yanaendelea taifa jirani la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambako kundi la Waasi wa M23 linaloaminika kuungwa mkono na utawala mjini Kigali linasonga mbele.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia sera ya Afrika alipozungumza na Shirika la Habari la Reuters pembezoni mwa mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini Geneva.

Waziri huyo Ray Collins, amesema Rwanda imeelezwa bayana msimamo wa Uingereza na sasa serikali mjini London inajiandaa kuiwekea vikwazo. Rwanda inakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuhusiana na madai ya kulisaidia kundi la M23 ambalo tangu mwezi Januari limeikamata miji Goma na Bukavu mashariki mwa Kongo.