1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yashawishika kifo cha Prigozhin

25 Agosti 2023

Idara ya ujasusi nchini Uingereza inasema kuna uwezekano mkubwa kwamba kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amefariki dunia.

Russland Yevgeny Prigozhin, Chef der Wagner-Gruppe abgestürzt
Picha: Dmitri Lovetsky/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Idara hiyo ya ujasusi imetoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X, ingawa imedai bado hakuna thibitisho la wazi kwamba Prigozhin alikuwa miongoni mwa abiria katika ndege iliyoanguka kwani kwa kawaida huchukua hatua kali za ulinzi.

Taarifa hiyo pia imesema kwamba kifo chake kitalipelekea kundi la Wagner kukumbwa na mtikisiko mkubwa.

Soma zaidi: Urusi baada ya kitisho cha uasi

Akitoa rambirambi kwa waliofariki katika ajali hiyo ya ndege hapo jana, Rais Vladimir Putin wa Urusi alionekana kuthibitisha ingawa si moja kwa moja kifo cha Prigozhin.

Putin alisema kwamba Prigozhin alikuwa mtu aliyekuwa na "kipaji" ila alifanya kile alichokiita "makosa makubwa."

Mnamo Juni, Prigozhin aliviongoza vikosi vyake katika jaribio la uasi wa kijeshi dhidi ya Moscow. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW