1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yasitisha utoaji wa Visa kwa mataifa manne

4 Machi 2026

Uingereza imesitisha kwa muda utoaji wa hati ya kusafiria ya Visa kwa raia kutoka nchi nne, huku waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Shabana Mahmood akiwashutumu kwa kutumia ukarimu wa Uingereza kuomba hifadhi.

 London 2025 | Shabana Mahmood
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Shabana MahmoodPicha: Thomas Krych/ZUMA/picture alliance

Mahmood amesema daima Uingereza itawakaribisha watu wanaokimbia vita na mateso, lakini kwamba mfumo wao wa kutoa Visa haupaswi kutumiwa vibaya.

Mahmood ameapa kudumisha utulivu na udhibiti kwenye mipaka yao.  

Visa za masomo kwa raia wa nchi hizo nne zimesitishwa, kama vile ilivyofanyika kwa visa za kazi kwa raia wa Afghanistan.

Kulingana na takwimu za Ofisi ya Mambo ya Ndani, asilimia 39 miongoni mwa watu 100,000 walioomba hifadhi mwaka wa 2025 waliwasilisha maombi ya hifadhi baada ya kuwasili Uingereza kupitia njia ya kisheria ya uhamiaji, kama Visa ya masomo.

Marufuku hiyo ya Visa itaanza rasmi kupitia mabadiliko ya sheria za uhamiaji kesho Alhamisi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW