1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza yatoa paundi milioni 61 kuzuia wahamiaji

Saleh Mwanamilongo
31 Desemba 2024

Serikali ya Uingereza imetangaza msaada wa paundi milioni 61 sawa na dola milioni 76 za Kimarekani kusaidia kukabiliana na majanga ya kibinadamu Mashariki ya Kati, Afrika na Asia.

Serikali ya Uingereza kutoa msaada wa paundi milioni 61 kuzuia wahamiaji
Serikali ya Uingereza kutoa msaada wa paundi milioni 61 kuzuia wahamiaji Picha: Dan Kitwood/Getty Images

Waziri wa Uingereza wa Maendeleo Anneliese Dodds amesema misaada ya kibinaadamu inaweza kutatua shida za uhamiaji kwa kupunguza haja ya watu kukimbia makaazi yao.

Dodds amesema mabadiliko ya tabia nchi, migogoro na umaskini uliokithiri vinachangia wimbi la uhamiaji.

Uingereza itatoa hadi paundi milioni 34 kushughulikia majanga ya kibinaadamu nchini Burkina Faso, Mali, Niger, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia, Myanmar na Bangladesh.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW