Uingereza yawawekea vikwazo maafisa wa Urusi.
17 Julai 2023Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, James Cleverly, ametangaza vikwazo hivyo 14 kabla ya hotuba yake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama sehemu ya kikao kuhusu vita nchini Ukraine.
Taarifa ya ofisi ya mambo ya nje imesema kuwa miongoni mwa waliowekewa vikwazo ni pamoja na Waziri wa Elimu wa Urusi, Sergey Kravtsov, na Kamishna wa Haki za Watoto wa nchi hiyo, Ksenia Mishonova.
Soma pia:Urusi: Mripuko katika daraja la Kerch ni tendo la ugaidi
Uingereza imewashtumu viongozi hao kwa jukumu lao la siri katika mpango wa Urusi wa uhamishaji huo wa kulazimishwa na kuongeza kuwa zaidi yawatoto 19,000 wa Ukraine wamehamishwa kwa kulazimishwa kuelekea Urusi ama kwa muda katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi.