Uingereza na Frontex wasaini mkataba wa ushirikiano
24 Februari 2024Matangazo
Uingereza imesaini mkataba na wakala wa ulinzi wa mpakani wa Umoja wa Ulaya Frontex kuimarisha ushirikiano wa mpakani na kupambana kwa pamoja dhidi ya uhamiaji usio halali.
Serikali ya Uingereza imesema hatua hiyo inanuiwa kudhibiti uhamiaji usio halali kupitia ujia wa English Channel kutoka bara la Ulaya.
Wakala wa Frontex umesema ushirikiano huo umejikita katika maelewano ya pamoja kwamba usimamizi mzuri wa mpaka unahitaji ushirikiano wa karibu katika mipaka.
Makubaliano hayo ni mwanzo wa awamu ya kupanga na maelezo bado hayajawekwa wazi. Frontex imesema pande zote zitashirikiana kwa pamoja kuainisha mipango mahususi ya ushirikiano.