Tembo waendelea kuuwawa Afrika
2 Septemba 2016Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa na jarida la Peer J siku ya jumatano utafiti huo umewahusisha tembo wanaopatikana katika ukanda wa savana kutokana na urahisi wa kuonekana ukilinganisha na tembo walioko porini na umeonyesha kuwa idadi ya tembo inazidi kushuka kutokana na kupungua kwa mazingira yao asilia pamoja, lakini sababu kubwa ya kupungua zaidi kwa tembo wa Afrika, ni Ujangili.
Ujangili ambao ulianza kushamiri mwaka 2005 umesababisha vifo vya zaidi ya tembo 30,000 mwaka uliopita
Inakadiriwa kuwa idadi jumla ya tembo walio katika ukanda wa savana katika nchi nchi 18 zilizojumuishwa ni 352,271 ambayo ni asilimia 93 ya tembo wote katika nchi hizo pamoja na kuwa utafiti huo haukuhusisha nchi kama vile Namibia ambako kuna idadi kubwa ya tembo lakini hawakutoa idadi kamili kwa ajili ya utafiti, Sudan Kusini na Jamhuri ya afrika ya kati ambako utafiti huo haukufanyika kutokana na migogoro inayoendelea katika nchi hizo
Nchi ambazo zimehusishwa katika utafiti huo ni pamoja na Botswana ambayo imechangia maeneo ya tafiti kwa asilimia 37, Zimbabwe imechangia kwa asilimia 23 na Tanzania asilimia 12
Angola, Tanzania na Msumbiji zaongoza kwa vifo vya tembo
Kupatikana kwa miili ya tembo waliokufa ni ishara ya kupungua kwa idadi ya tembo huku ripoti hiyo ikizitaja nchi zinazoongoza kuwa vifo vya wanyama hao ni pamoja na Cameroon, Msumbiji, Angola na Tanzania. wakati nchi ambazo zinaongoza kwa pembe za ndovu ni Msumbiji, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Paschal Shelutete meneja wa mawasiliano wa shirika la hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA shirika ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia maeneo yaliyotengwa kisheria kama hifadhi za Taifa nchini humo anasema Tanzania kwa upande wake imeanza kufanikiwa kupunguza ujangili kwa mikakati mbalimbali ya kukabiliana nao hii ikiwa inajumuisha kutenga bajeti kubwa kwa ajili ya kuliwezesha shirika hilo kuwa kufanya doria katika maeneo ya hifadhi
Kwa mujibu wa ripoti hiyoya Jumatano, ikiwa ujangili dhidi ya tembo utaendelea utasababisha kutokuwepo kabisa kwa wanyama hao katikia nchi za Mali,Chad na Cameroon wakati ikizitaja nchi za Botswana, Afrika kusini, Zambia na Zimbabwe ambazo zina idadi kubwa ya tembo kuwa hazijaathiriwa sana na ujangili
Mwandishi: Celina Mwakabwale
Mhariri: Gakuba Daniel