1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani bado inakabiliana na mafuriko

3 Januari 2024

Ujerumani inaendelea na kukabiliana vikali na mafuriko katika kipindi hiki ambacho mamlaka ya hali ya hewa ikitabiri mvua kuendelea kunyesha hadi mwishoni mwa juma.

Hochwasser in Deutschland | Niedersachsen Hannover
Hali ya mafuriko katika baadhi ya maeneo ya mji wa HannoverPicha: Andre Germar/IMAGO

Hali hiyo inaongeza mashaka kwa mamlaka.Mashamba kadhaa katika jimbo la kaskazini la Lower Saxony yamejaa maji, huku kukishuhudiwa mafuriko ya mto Elber. Baadhi ya maeneo ya majimbo ya North Rhine-Westphalia, Saxony-Anhalt na Thuringia kadhalika yameathirika. Kwa mujibu wa ofisi ya Huduma ya Hali ya Hewa ya Ujerumani (DWD), mvua kubwa ni inatarajiwa katika majimbo ya Lower Saxony hadi Alhamisi na Thuringia hadi Ijumaa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW