China yadaiwa kuendesha shughuli za polisi nchini Ujerumani
15 Mei 2023Matangazo
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Ujerumani ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa, mamlaka za usalama zinashuku uwepo wa vituo viwili vya polisi vya China nchini Ujerumani.
Msemaji huyo amefafanua kwa, vituo hivyo vya polisi vya China havikuwepo kwenye eneo maalum bali ni vya kuhamahama na kwamba raia wa China na wasio Wachina wamekuwa wakifanya "kazi rasmi" kwa niaba ya Beijing.
Ujerumani iliitaka China mnamo mwezi Novemba kufunga vituo vyake vya polisi vilivyoko nje ya mipaka yake.
Ubalozi wa China mjini Berlin haukujibu mara moja ombi la kutoa kauli yake juu ya suala hilo.