1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Chuki kwa waislamu iliongezeka maradufu 2023

24 Juni 2024

Muungano wa Ujerumani unaopinga chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu, umesema leo kwamba uhalifu unaosababishwa mitizamo ya chuki dhidi ya waislamu uliongezeka zaidi ya mara mbili nchini Ujerumani mwaka uliopita.

Mitaa ya mji mkuu wa Ujerumani, Berlin
Vitendo vya chuki dhidi ya waislamu nchini Ujerumani vilipindukia vitano kila siku mwaka 2023.Picha: TOBIAS SCHWARZ/AFP/Getty Images

Kundi hilo limesema limerekodi jumla ya visa 1,926, ikiwa ni ongezeko la kiasi cha visa vitano vya kila siku kwa wastani na ongezeko la zaidi ya visa 1,000 vya mwaka uliopita.

Mkurugenzi wa kundi hilo lijulikanalo pia kama Claim, Rima Hanano amedai  ubaguzi dhidi ya Waislamu haujawahi kukubalika kwenye jamii, kama ilivyo sasa.

Visa vilivyozungumziwa vilikuwa vya mashambulizi ya maneno au matusi, ubaguzi, lakini pia vitisho na kulazimishwa. Claim pia ilijumuisha majaribio manne ya mauaji na visa vitano vya uchomaji moto.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW