1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haitingishwi na machafuko ya dunia - Scholz

31 Desemba 2023

Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, Kansela Olaf Scholz amesema Ujerumani italazimika kubadilika mbele ya ulimwengu "usio na utulivu na mkali zaidi" lakini alikuwa na uhakika kuwa nchi hiyo itavuka salaama changamoto hizo.

Ujerumani | Kansela Scholz | Hotuba ya mwaka mpya 2023/2024
Scholz amesema nguvu ya Ujerumani iko katika utayari wake wa maelewanoPicha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Katika ujumbe wake wa Mwaka Mpya, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekiri juu ya hali ngumu ya kimataifa lakini ameonyesha imani kwamba "Ujerumani itashinda."

"Mateso mengi; umwagaji mwingi wa damu. Ulimwengu wetu umekuwa sehemu isiyotulia na kali zaidi. Inabadilika kwa kasi ya kustaajabisha," Scholz alisema, kulingana na maandishi ya hotuba yake iliyotolewa na ofisi yake kabla ya kutangazwa kwenye mkesha wa mwaka mpya.

"Matokeo yake ni kwamba sisi pia, inabidi tubadilike. Hili ni jambo la kutia wasiwasi kwa wengi wetu. Kwa baadhi, pia linasababisha kutoridhika. Nalitilia maanani hilo."

Kiongozi huyo wa Ujerumani, hata hivyo, alitoa maoni ya matumaini na kuangazia vikwazo ambavyo nchi hiyo ilifanikiwa kushinda mnamo 2023, ndani na kimataifa.

"Nguvu zetu ziko katika utayari wetu wa kuafikiana - katika juhudi tunazoweka kwa ajili ya mtu mwingine," Scholz alisisitiza.

Kansela Scholz amesema Ujerumani imefanikia kuziwoa mdororo wa kiuchumiPicha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Uchaguzi wa Marekani huenda ukawa na athari kubwa

Huku chaguzi nyingi muhimu zikifanyika duniani kote mwaka wa 2024, hasa Marekani, Uingereza, India na Bunge la Ulaya, Scholz alisisitiza umuhimu wa chaguzi hizi - hasa Marekani - wakati ambapo vita vinaendelea nchini Ukraine na Mashariki ya Kati.

Kansela huyo amesisitiza kuwa nguvu ya Ujerumani iko katika Umoja wa Ulaya. "Ni muhimu sana kwa Ulaya kuibuka ikiwa imeungana na imara kutoka kwenye uchaguzi wa Ulaya katika mwaka ujao," alisema.

Soma pia:Je, ukomo wa deni la Ujerumani ni nini hasa? 

"Hata hivyo, vita vya Urusi mashariki mwa bara letu havijakwisha. Wala mzozo wa silaha katika Mashariki ya Kati haujamalizika. Mwaka ujao pia utashuhudia uchaguzi wa rais nchini Marekani, ambao unaweza kuwa na madhara makubwa - ikiwa ni pamoja na kwetu hapa Ulaya."

'Tulidhiti mdororo wa kiuchumi'

Huku mfumuko wa bei ukishuka kutoka wastani wa asilimia 7.9 mwaka 2022 hadi asilimia 3.2 mnamo Novemba 2023, kiwango cha chini kabisa katika miaka miwili, Scholz alizungumza juu ya mtazamo mzuri zaidi wa kiuchumi kuliko mwaka mmoja uliopita - hata wakati kiwango cha mfumuko wa bei cha Ujerumani bado ni cha juu zaidi. kuliko wastani wa asilimia 2.4 katika kanda ya Euro.

Pia alizungumzia usambazaji wa gesi ya Ujerumani iliyojazwa tena, ambayo aliielezea kama "iliyojaa hadi ukingo" na kusema nchi hiyo iliepuka kudorora kwa uchumi.

"Mnakumbuka tulipokuwa mwaka mmoja uliopita?" Scholz aliuliza. "Wataalamu wengi walikuwa wametabiri kushuka kwa uchumi kwa asilimia tatu, nne, tano. Wengi walihofia kuwa bei zingeendelea kupanda. Kulikuwa na wasiwasi kuhusu kukatika kwa umeme na kukosekana kwa joto katikabaadhi ya majumba.

Soma pia:Ujerumani: Waziri wa zamani wa fedha Wolfgang Schäuble afariki dunia 

"Mambo yamekuwa tofauti," alihitimisha. "Mfumuko wa bei umepungua. Mishahara na pensheni vinapanda. Mifumo yetu ya kuhifadhi gesi imejaa hadi ukingoni kwa msimu wa baridi."

"Tulizuia mdororo huo wa uchumi," Scholz aliongeza. "Tuliokoa nishati, na tulifanya maandalizi kwa wakati. Sote tulifanya - kwa pamoja."

Ujerumani na sifa ya uzalishaji bora wa bidhaa

03:48

This browser does not support the video element.

Matarajio ya mwaka 2024

Scholz, ambaye ni kiongozi wa chama cha Social Democrat cha Ujerumani (SPD), pia alisema serikali ya muungano itaweka kipaumbele katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara na reli katika kile alichoeleza kuwa ni hitaji la "kuwekeza kwa nguvu katika siku zijazo."

Chama cha SPD kinatawala kwa pamoja na chama cha Kijani, na kile cha Kiliberali, Free Democrats (FDP).

"Kama mtu yeyote atakuwa amegundua nani anasafiri kwa treni siku hizi, au anakaa kwenye msongamano wa magari kwenye njia ya daraja linalobomoka, nchi yetu imerudishwa nyuma kwa muda mrefu sana," alisema. "Ndio maana tunawekeza sasa - katika barabara nzuri na reli bora."

Soma pia: Scholz: Uamuzi wa EU unapaswa kuwa ishara pia kwa Putin

Lakini alikiri kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba mnamo Novemba kwamba fedha za kukabiliana na athari za janga ambazo hazijatumika hazingeweza kutumika tena kwa miradi ya mazingira na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, "hatutaweza kutekeleza mipango yote tuliyotarajia."

Scholz anaamini kwamba kila mtu nchini Ujerumani ana jukumu muhimu, na kwa kuheshimiana, "hatuhitaji kuwa na hofu juu ya siku zijazo."

"Basi mwaka 2024 utakuwa mwaka mzuri kwa nchi yetu hata kama baadhi ya mambo yatatokea tofauti na vile tunavyowazia leo, usiku wa kuamkia mwaka mpya."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW