1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haitoweka sheria kwa lengo la NATO kijeshi

18 Agosti 2023

Serikali ya Ujerumani haitaki kuweka sheria kwa ajili ya kulifikia lengo la matumizi ya kijeshi la Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Haya ni kwa mujibu wa duru zilizo karibu na serikali.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.Picha: Kay Nietfeld/picture alliance/dpa

Duru hizo zimeliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba kuelekea maamuzi muhimu ya baraza la mawaziri, serikali imekiondoa kutoka kwenye rasimu ya sheria ya bajeti, kipengee kinachoitaka Ujerumani kutumia asilimia mbili ya pato lake jumla kwa ulinzi.

Mapema wiki hii, vyombo vyengine vya Ujerumani pia viliripoti taarifa hiyo.

Maazimio ya jumuiya ya NATO yanawataka wanachama wake wote kutumia kiwango hicho kwenye matumizi yake ya kijeshi ingawa Ujerumani na mataifa mengine ya Ulaya Magharibi hayajakifikia kiwango hicho.

Hivi majuzi, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema serikali yake itatumia kiwango hicho cha fedha katika kipindi cha muda mrefu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW