Ujerumani imeyaaga mashindano ya kombe la dunia ya wanawake
10 Julai 2011Matangazo
Katika mashindano yanayoendelea ya Kombe la Dunia la wanawake, mabingwa watetezi Ujerumani, wametolewa kwenye mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Japan kunako dakika 120 ya mchezo huo.
Ushindi wa Japan mjini Wolfsburg umezima matumaini ya Ujerumani kujinyakulia mara ya tatu mtawalia, taji la mashindano haya.
Wakati huo huo, Japan imefuzu kwenye nusu fainali za mahsindano hayo na inatarajiwa kupambana na Sweden au Australia.
Mapema hapo jana, Ufaransa iliifunga timu ya Uingereza kupitia mikwaju ya penalti mjini Leverkusen na pia kufanikiwa kuingia kwenye nusu fainali hizo. Ufaransa sasa itakabiliana na Marekani au Brazil.
Mwandishi: Maryam Abdalla/Dpae/Zdf
Mhariri:Martin,Prema