1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani, India zalenga kuimarisha ushirikiano wa ulinzi

Sylvia Mwehozi
25 Oktoba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anataka kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi na India na kuyasogeza karibu majeshi ya nchi hizo mbili.

Kansela Olaf Scholz (SPD) akizungumza na Narendra Modi (kulia), Waziri Mkuu wa India (kumbukumbu)
Kansela Olaf Scholz (SPD) akizungumza na Narendra Modi (kulia), Waziri Mkuu wa India (kumbukumbu)Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Scholz ametoa kauli hiyo mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi leo Ijumaa.Kansela huyo amenukuliwa akisema, "Na bila shaka, tunataka makubaliano ya biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na India. Serikali yangu inasukuma maendeleo na hitimisho la haraka, na nina hakika kwamba ikiwa tutafanyia kazi pamoja, juu ya hili." Waziri Mkuu Modi, hili linaweza kufanikiwa ndani ya miezi, badala ya miaka. Scholz aliyeambatana na baadhi ya mawaziri anaongoza ujumbe wa ngazi ya juu mjini New Delhi, akitumai kuwa ufikiaji wa soko kubwa la India unaweza kupunguza utegemezi wa Ujerumani kwa China