Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani na Kenya wameweka wazi msimamo wao kuhusu umuhimu wa kuimarisha Umoja wa Mataifa kama nguzo kuu ya usimamizi wa amani na utatuzi wa migogoro duniani, wakati kukiwa na wasiwasi unaotokana na taarifa kwamba Rais wa Marekani Donald Trump anapanga kuanzisha chombo kipya cha kimataifa kitakachoshughulikia masuala ya amani.