Ujerumani kuanza chanjo katika ngazi ya kaya.
20 Machi 2021Chanjo nyingine ya ziada itatolewa pia katika mikoa ya taifa hilo inayopakana na Ufaransa na Jamhuri ya Czech.
Hapo Jana Ijumaa, serikali kuu na za majimbo ya Ujerumani zilifanya mazungumzo kuhusu chanjo ya virusi vya corona baada ya Shirika la Uratibu wa Madawa la Ulaya (EMA) kutoa taarifa kwamba chanjo ya AstraZeneca ni salama kwa matumizi.
Maeneo ya mipakani ya Ujerumani kutolewa chanjo za papo kwa papo.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wa majimbo wametoa ridhaa ya madaktari wa kawaida katika ngazi ya kaya kuratibu zoezi hilo la utoaji wa chanjo baada ya sikuu ya Pasaka, huku kukiwa na dozi ya ziada zikitolewa papo kwa papo katika maeneo ya majimbo ya mipakani ya Ujerumani.
Kwa muda mrefu kampeni ya utoaji wa chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona nchini Ujerumani imekuwa ikikosolewa kutokana na kuchelewa kwake.
Mkakati mpya wa utoaji chanjo katika majimbo.
Kwa mujibu wa makubalino hayo mapya, miongoni mwa mambo ambayo yametiliwa mkazo ni pamoja na hatua za utekelezaji zitaanza kuchukuliwa katika majuma yanayofuata. Zoezi la utoaji wa chanjo linatarajiwa kuanza baada ya pasaka lakini kwa makadilio ya kiasi.
Na kama ilivyo utaratibu wa utaoji wa chanjo hizo zingatio kubwa hata katika ngazi hizo za kawa litakuwa kwa watu ambao wapo katika mazingira hatarishi ambapo takribani chanjo milioni 15.4 zitakuwa tayari zimetawanywa ifikapo Aprili.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya ya Ujerumani ya Robert Koch, zaidi ya watu milioni 3 nchini Ujerumani tayari wamekamilisha mchakato wa kujipatia chanjo ya COVID-19 na wengine karibu milioni 7 wameanza dozi ya kwanza.
Chanzo: DW