Ujerumani kuanza tena ushirikiano na shirika la UNRWA
24 Aprili 2024Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani pamoja na wizara ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo.
Uamuzi huo unafuatia uchunguzi uliofanywa na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ufaransa Catherine Colonna, kuhusu madai ya Israel kwamba baadhi ya wafanyakazi wa UNRWA walihusika katika shambulio la Oktoba 7 dhidi ya nchi hiyo.
Uchunguzi huo usioegemea upande wowote siku ya Jumatatu ulihitimishwa kwa ripoti iliyobaini kwamba Israeli haikuwa na ushahidi wowote kuthibitisha madai yake.
Wizara za Ujerumani zimehimiza shirika la UNRWA kutekeleza haraka mapendekezo ya ripoti hiyo ya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi wa ndani na kuboresha usimamizi wa nje wa miradi yake.