Ujerumani kuchuana na Ureno leo
16 Juni 2014Matangazo
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema itakuwa vigumu kuilaza timu yake iwapo wachezaji wake watatumia uwezo wao. Kwa upande wa Ureno pia watakuwa wanategemea pakubwa mchango wa mchezaji wao nyota Christiano Ronaldo kuibuka na ushindi katika mechi hiyo ya makundi. Marekani nayo itachuana na Ghana leo usiku katika mechi ya kundi G. Timu nyingine ya Afrika- Nigeria itakuwa uwanjani dhidi ya Iran katika ya kundi F.