1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasema itaimarisha uhusiano wake na Taiwan

14 Januari 2024

Mchakato huo utafanyika kulingana na sera ya Ujerumani inayozingatia China moja

Taiwan | Präsidentschaftswahlen
Picha: Kyodo/picture alliance

Ujerumani imesema inapendelea kuimarisha uhusiano wake na Taiwan baada ya kufanyika uchaguzi nchini humo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ameeleza kuwa mchakato huo utafanyika kulingana na sera ya Ujerumani ya China moja.

Kushoto mbel3: Rais mteule wa chama cha kidemokrasia, DPP, Lai Ching-te. Kulia mbele: Makamu wa rais wa chama cha DPP wakisherehekea ushindi wao katika uchaguzi wa rais wa Taiwan uliofanyika januari 13. 2024. Taiwan imemchagua Lai Ching-te mwenye umri wa miaka 64 na anatarajiwa kuapishwa nwezi Mei. Chama cha DPP kitaingoza Taiwan mara tatu mfululizo.Picha: Ichito Ohara/The Yomiuri Shimbun/AP/picture alliance

Chama tawala Taiwan chashinda uchaguzi wa rais

Kwa mujibu wa sera hiyo Taiwan haitatambuliwa kuwa nchi huru na kwamba uhusiano wa kidiplomasia utadumishwa na China tu.Marekani kutuma ujumbe usio rasmi Taiwan baada ya uchaguzi

Katika uchaguzi wa rais uliofanyika mnamo wiki hii mjumbe wa chama cha kidemokrasia, DPP, Lai Ching-te mwenye umri wa miaka 64 alishinda kwa kupata asilimia takriban 40 ya kura. Chama cha Lai kinatetea sera ya Taiwan ya kuwa na utambulisho wake, ingawa haijajitangazia uhuru.

Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi alipotoa hotuba ya mwaka mpya kwa taifa lake mnamo Desemba. 29.2023 mjini Beijing. Picha: Yao Dawei/Xinhua News Agency/picture alliance

Jeshi la China liko tayari kuvunja njama za Taiwan kujitenga

China inayosisitiza kuwa Taiwan ni sehemu ya himaya yake inakizingatia kisiwa hicho kuwa sehemu iliyojitenga. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani ameeleza kuwa Ujerumani imekuwa na uhusiano mzuri na wa karibu na Taiwan kwa miaka mingi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW