Ujerumani kutanua mifumo ya kijamii nchi za Sahel
9 Oktoba 2023Matangazo
Wizara ya Maendeleo imetangaza leo Jumatatu kwamba fedha kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF, na lile la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, zitaongezwa kwa kiasi cha dola milioni 42.
Soma pia: Ujerumani kuwa nchi ya pekee barani Ulaya kuingia kwenye mdororo wa uchumi 2023
Fedha hizo zitatumika kusaidia nchi kama vile Mauritania iliyo kaskazini-magharibi mwa Afrika, ambayo kwa sasa imo kwenyejuhudi kubwa za kuwachukua wakimbizi wengi kutoka nchi jirani ya Mali na inajaribu kuwajumuisha katika mifumo yake ya kijamii.
Eneo la Sahel ni mojawapo ya maeneo maskini na linalokabiliwa na ukame mkubwa duniani.