Ujerumani kurefusha muda wa viwanda vya nyuklia
30 Agosti 2010Hata hivyo,ni lazima kuhakikisha usalama wa viwanda hivyo vya nyuklia. Kwa maoni yake, utaratibu wa kurefusha muda wa viwanda hivyo, uandaliwe kwa njia ambayo hautohitaji kuidhinishwa na baraza la waakilishi wa serikali za majimbo "Bundesrat."
Baadhi ya majimbo yanayoongozwa na chama cha kisoshalisti cha SPD yametishia kuifikisha kesi hiyo katika mahakama ya katiba. Kiongozi wa SPD, Sigmar Gabriel amemtuhumu Merkel kuridhia sera za washawishi wa kampuni za nishati ya nyuklia. Amesema, kwa kukutaka kurefusha muda wa viwanda hivyo, Kansela Merkel anauza usalama wa umma. Hata chama cha mazingira cha Kijani na Die Linke cha mrengo wa kushoto vimemkosoa Merkel.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,anataka kurefusha muda wa viwanda vya nishati ya nyuklia kwa hadi miaka kumi na tano.Amesema, kuambtana na ripoti ya wataalamu, kiufundi, huo ni muda unaoingia maanani.
Hata hivyo, usalama wa viwanda hivyo vya nyuklia unapaswa kuhakikishwa.Kwa maoni yake,utaratibu wa kurefusha muda wa viwanda hivyo, uandaliwe kwa njia ambayo hautohitaji kuidhinishwa na baraza la waakilishi wa serikali za majimbo "Bundesrat."
Baadhi ya majimbo yanayoongozwa na chama cha kisoshalisti cha SPD yametishia kuifikisha kesi hiyo katika mahakama ya katiba. Kiongozi wa SPD, Sigmar Gabriel amemtuhumu Merkel kuridhia sera za washawishi wa kampuni za nishati ya nyuklia. Amesema, kwa kukutaka kurefusha muda wa viwanda hivyo, Kansela Merkel anauza usalama wa umma. Hata chama cha mazingira cha Kijani na Die Linke cha mrengo wa kushoto vimemkosoa Merkel.
Mwandishi/P.Martin/ZPR