1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuruhusu Wakenya kupata fursa za ajira zaidi

22 Julai 2024

Kenya na Ujerumani zitatia saini makubaliano ya wakenya kupata ajira nchini Ujerumani huku kenya ikilenga kuimarisha mikakati yake ya kitaifa ili kukabiliana na tatizo la ukosefu mkubwa wa ajira.

Berlin, Ujerumani | Kenya | Rais William Ruto na Kansela Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Kansela Olaf Scholz akiwa na Rais wa Kenya William Ruto.Picha: Political-Moments/IMAGO

Taifa la Kenya sawia na mataifa mengine duniani linakabiliwa na changamoto ya kiuchumi hatua ambayo inaathiri viwango vya ajira miongoni mwa raia wake.

Kulingana na takwimu za asasi inayosimamia data za kitaifa - KNBS ya mwaka 2023, takriban wakenya milioni 2.97 hawana ajira, zaidi ya nusu ya idadi hii wakiwa vijana wa umri kati ya miaka 20 - 29, idadi hii inadhihirisha ukosefu mkubwa wa ajira miongoni mwa vijana ambao hasaa ni kizazi cha nguvu kazi.

Katika mkakati wa kudhibiti ongezeko la ukosefu wa ajira miongoni mwa raia wa Kenya, katibu mkuu wa wizara ya kazi na Uimarishaji Ujuzi Shadrack Mwadime amesema Kenya itatia saini makubaliano ya usafirishaji wa ajira na serikali ya Ujerumani wizara ya kitaifa ya leba ikiendelea na ukaguzi wa ujuzi wa watu takriban alfu 40 kupitia mtandao wa Mamlaka ya Uajiri wa kitaifa.

"Tupo karibu kutia saini makubaliano ya ajira na Ujerumani mwezi Septemba, tumekuwa na awamu mbili za majadiliano ya kwanza Ujerumani na nyingi hivi karibuni"

Soma pia:Idadi ya watu wasio na ajira Ujerumani yaongezeka mwezi Juni

Mwadime anasema, miongoni mwa sababu za idadi kubwa ya vijana kuonekana kwenye maandamano ni dhihirisho tosha kuwa, swala la ukosefu wa ajira lipo juu zaidi na hivyo kuna haja ya uwajibikaji ili kutwaa baadhi ya nafasi za ajira zilizopo kwenye mataifa ya Magharibi.

Kuwafikia hasaa vijana wengi ili kuwaandaa kwa ajira zinazojitokeza, Mwadime ameeleza kuwa, wanatumia mtando wa Mamlaka ya Uajiri wa kitaifa wakiwahimiza kubuni akaunti za kibinafsi huku ushirikiano zaidi ukidumishwa pia na wizara ya vijana ikizingatiwa mpango unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa Nyota na kuweka makubaliano ya kuwashirikiza zaidi vijana.

"Baadhi yao wamewasiliana na sisi baada ya kugundua nchini Kenya tuko na vijana wenye ujuzi mkubwa, na walio na nidhamu na hivi ndivyo vigezo tunavyotangaza huko nje"

Vijana waukaribisha mpango huo

Baadhi ya vijana akiwemo Emmanuel Kiprotich wanapongeza hatua ya mikati ya ajira nchi za nje ila wanaendekeza serikali kuweka mikakati itakayowahakikishia usalama wao katika ajira hizo wakirejelea baadhi ya misukosuko inayoshuhudiwa hasaa kwa raia wa kingeni katika nchi zingine na pia kuhimiza serikali kuweka mazingira bora ya biashara na nafasi za ajira nchini ili kuimarisha nafasi hizi nchini Kenya.

Uhaba wa mafundi Ujerumani, jee wahitaji kuwa na nini kuziwahi?

01:32

This browser does not support the video element.

"Ukiniambia niende Ujerumani ama niende china, kuna vitu gani ambavyo serikali itaniasaidia nikiwa nimefika huko katika nafasi hiyo ya kazi, nitaishije huko."

Soma pia:Wafanyakazi wahamiaji wanahofia ubaguzi wa rangi Ujerumani?

Kando na Ujerumani, Kenya vile vile inaendelea kuweka mikakati kuweka makubaliano na mataifa 19 yakiwemo ya  Bara Ulaya na Bara Asia.

Mamlaka ya Kitaifa ya Uajiri kupitia Mkurugenzi Mkuu Edith Okoki imeahidi kutoa mafunzo kwa watakaopata ajira za nchi za nje.

"Utaonyeshwa vile kuleta pesa yako nyumbani, kuna hiyo mafunzo tutawapatia pia."

Kulingana na takwimu za asasi simamizi ya data KNBS viwango vya ukosefu wa ajira nchini Kenya vinasimamia katika asilimia 6.6.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW