1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Ujerumani kuwapokea WaAfghani 535 kutoka Pakistan

18 Desemba 2025

Ujerumani imetangaza Alhamisi kuwa itawapokea raia wa Afghanistan wapatao 535 waliokuwa wameahidiwa kupewa hifadhi nchini Ujerumani lakini hadi sasa wakiwa wamekwama katika hali ya sintofahamu nchini Pakistan.

Berlin | Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Alexander Dobrindt
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Alexander Dobrindt akizungumza na polisi mjini BerlinPicha: Sebastian Rau/photothek.de/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Alexander Dobrindt amesema wanatarajia kukamilisha mchakato wa kulishughulikia suala hilo mnamo mwezi huu wa Desemba, ili kuwaruhusu watu hao kuwasili nchini Ujerumani. Mpango huo uliidhinishwa na utawala uliopita na Kansela Friedrich Merz aliusitisha mara tu alipoingia madarakani.

Watakaonufaika na mpango huo ni watu walioshirikiana na jeshi la  Ujerumani nchini Afghanistan wakati wa vita dhidi ya Taliban, au wale waliotajwa kuwa katika hatari kubwa baada ya Taliban kurejea madarakani mnamo mwaka 2021, ikiwa ni pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari pamoja na familia zao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW