1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani Mashariki na Nicaragua

5 Novemba 2009

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani iliunga mkono mapinduzi ya kisandinista nchini Nicaragua pia kwa kutoa mafunzo kwa vijana wa nchi hiyo iliyopo katika Amerika ya Kati.

Einmarsch der Sandinisten in Managua 1979, 19. Juli,A pair of jubilant Sandinista Guerrillas ride into Managua on a tank flying a guerrilla flag Thursday, June 19, 1979 in Managua, Nicaragua. Seven hundred guerrillas paraded in from Leon to celebrate the fall of Gen. Anastasio Somoza's regime and the end of more than 40 years of rule by the Somoza family. (AP Photo/Jennings)
Wasandinista walipoingia Managua 1979 kufanikisha mapinduzi nchini humoPicha: AP

Lakini mambo yalibadilika haraka sana baada ya ukuta wa Berlin kuangushwa.

Baada ya wasandinista kufanikiwa kuleta mapinduzi nchini Nicaragua mnamo mwaka 1979 Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani yaani sehemu iliyokuwa inaitwa Ujerumani Mashariki hapo awali ilianza kuvutiwa na mapinduzi hayo kwani yalikuwa na mwelekeo wa kisoshalisti.

Ujerumani Mashariki iliyaunga mkono mapinduzi hayo pia kwa kutoa mafunzo kwa vijana wa Nicaragua. Ujerumani ya Mashariki ilitoa misaada kwa nchi hiyo na yenyewe ilipata fedha za kigeni.

Ujerumani Mashariki pia ilitoa mafunzo kwa vijana wa Nicaragua kwa lengo la kuwapiga msasa wa kiitiikadi vijana hao.

Hayo yalifanyika wakati JJU ilipokuwa katika mfungamano wa nchi za kikomunisti za Ulaya ya Mashariki.

Carlos Ampie Loria alikuwa miongoni mwa wanafunzi walioalikwa kufanya mafunzo nchini Ujerumani Mashariki. Alisoma kwa bidii ili baadae atoe mchango katika kufanikisha mapinduzi nchini Nicaragua.

Carlos Loria anakumbuka.

Kwetu sisi ilikuwa wazi: tulijifunza kwa manufaa ya nchi yetu. Tulijifunza kwa bidii ili kufanikisha mapinduzi. Tulikuwa na wajibu wa kufanya hivyo.Tulikuja kujifunza na baada ya kumaliza turejee."

Kijana huyo alikwenda Ujerumani Mashariki mnamo mwaka 1984.Alianza mafunzo katika mji maarufu wa bandari Rostock.Alifanya mafunzo ya ufundi wa radio na televisheni.

Licha ya matatizo ya hali ya hewa,tofauti za chakula na utamaduni kwa jumla Carlos Lorian alifanya masomo yake kwa bidii kwa lengo la kufanikisha mapinduzi nyumbani.

Mapinduzi yaliyoletwa mnamo mwaka 1979 baada ya dikteta Somoza kutimuliwa madarakani.

Lengo la mapinduzi lilikuwa kugawa ardhi upya,kuanzisha kampeni ya kufuta ungumbaro na ,kuleta mageuzi ya kijamii.Licha ya tofauti za kiitikadi baina ya Nicaragua na JKU , viongozi wa JKU walisisitiza mshikamano na Nicaragua.Ujerumani Mashariki ilikuwa nchi ya kwanza ya Ulaya Mashariki kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Nicaragua.JKU iliunga mkono mapinduzi ya Nicaragua kwa misaada ya maandeleo lakini pia iliipa nchi hiyo silaha ili kuweza kupambana na wapinzani waliokuwa wanaitwa Kontra.Lakini misaada hiyo ilifikia mwisho tarehe 9 mwezi Novemba mwaka 1989. Kilichofuata kilikuwa ni kuangushwa kwa Kuta la Berlin.

Carlos alisema wakati huo.

Nilipigwa butaa.Kwa sababu nilijua kwamba ndoto yetu ilitoweka.

Hali haikuwa rahisi kwa vijana wa Nicaragua waliorejea nchini mwao. Walionekana kama maadui. Lakini mnamo mwaka 2005 Carlos alirejea Ujerumani, siyo kwa ziara fupi, bali kuishi hapa nchini daima.Lakini amesema wakati wote ataendelea kuunga mkono mradi kama ule ulioanzishwa nchini Nicaragua.

Mwandishi/Ina Rottscheid/ZA

Imerafsiriwa/Mtullya Abdu.

Mhariri/.