MigogoroUjerumani
Ujerumani: Mchakato wa amani Gaza utakuwa mgumu
1 Oktoba 2025
Matangazo
Hata hivyo Wadephul ambaye alizungumza na shirika la habari la Funke na matamshi yake kuchapishwa, amesema huenda usianze kutekelezwa mara moja.
Waziri huyo amesema kwamba bado kuna maswali mengi magumu kuhusiana na namna mpango huo utakavyotekelezeka, ikiwa ni pamoja na namna Gaza itakavyotawalika, hakikisho la usalama na hata namna misaada ya kiutu itakavyorejeshwa Gaza na kusisitiza kwamba utakuwa ni mchakato mgumu.
Alipozungumza na kituo cha utangazaji cha ZDF jana Jumanne alisema pia kuna mashaka ikiwa mataifa ya Kiarabu na kundi la Hamas watakubaliana nao na kuongeza kuwa atakwenda Qatar siku ya Jumapili akisistiza kuitumia vyema fursa hii kumaliza mateso dhidi ya watu wa pande zote mbili.