1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Michezo kuendelea wakati shughuli zikifungwa

15 Desemba 2020

Michezo ya kulipwa nchini Ujerumani ikiongozwa na Ligi Kuu ya Bundesliga itaendelea kuanzia Jumatano wakati wa zuio la shughuli muhimu za umma likianza kutekelezwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya corona.

Deutschland Fußball Bundesliga FC Augsburg vs FC Schalke 04
Picha: dpa/picture alliance

Michezo ya kulipwa nchini Ujerumani ikiongozwa na Ligi Kuu ya kandanda - Bundesliga itaendelea kuanzia Jumatano wakati wa zuio la shughuli muhimu za umma likianza kutekelezwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizo ya virusi vya corona. Waziri wa Afya Jens Spahn amethibitisha katika mkutano na waandishi wa habari kuwa licha ya kusambaa kwa maambukizo, michezo itaendelea bila mashabiki viwanjani. Waziri huyo ameongeza kuwa michezo ya kulipwa pia haitaathiri uwezo wa upimaji ambao amesema utakuwa wa hali ya juu kabisa. Michezo ya kulipwa ilisitishwa wakati wa zuio la kwanza la shughuli za umma kabla ya kurejea tena Mei chini ya taratibu kali za usafi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW